News News

Back

ACACIA YAFUTWA RASMI DSE

18 Dec 2019
MWANANCHI
Image

Dar es Salaam

Baada ya miaka minane ya kudumu katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), kampuni ya Acacia yafutwa rasmi Novemba 18, 2019.

Kampuni hiyo iliyoorodheshwa DSE Desemba 2011 ikijulikana kama African Barrick Gold (ABG) kabla haijabadili jina na kuitwa Acacia Novemba 2014, imeondolewa sokoni hapo baada ya kukamilisha utaratibu wa kufutwa.

“Acacia ilifutwa katika Soko la Hisa London (LSEG) tangu Septemba. DSE itaifuta kuanzia leo Novemba 18, 2019”, inasomeka taarifa ya DSE iliyowekwa kwenye tovuti yake.

Kufutwa kwa kampuni hiyo, taarifa zinaonyesha kutapunguza ukubwa wa mtaji wa soko hilo kutoka Sh 19.67 trilioni uliokuwapo mwishoni mwa wiki iliyopita hadi Sh 16.94 trilioni.

Wakati ukubwa wa mtaji wa soko zima ukipungua,ule wa kampuni za ndani, Sh9.01 trilioni hautabadilika.

“Hii inamaanisha ndio mwisho wa kuwa na kampuni ya Acacia katika soko letu. Walituandikia nasi tumewakubalia kuwafuta, “ alisema Moremi.