News News

Back

KILO YA SUKARI 4,000/- KIBAHA

22 Apr 2020
Habari leo Aprili 2010
Image

Wafanyabiashara wilayani Kibaha wameanza kupandisha bei ya sukari kutoka Sh 2,800 hadi 4,000 kwa kilo, wakidai nao wananunua kwa bei kubwa.

 

Kutokana na hali hiyo, wananchi wameiomba serikali kushughulikia suala hilo la upandaji wa bei ya sukari.  Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya wananchi walisema kuwa bei hiyo ni mzigo mkubwa, hivyo ni bora serikali idhibiti wauzaji hao.

 

Godfrey Lucas alisema wanashangaa kuona wakiambiwa kuwa sukari hakuna na bei imepanda.

 

Kwamba hali ya sasa ni mbaya, hasa ikizingatiwa sukari ni moja ya vitu muhimu kwenye matumizi ya vyakula.

 

“Tumeambiwa hakuna tatizo la sukari nchini, lakini mbona bei imepandishwa? Kuna haja ya serikali kuchukua hatua kama kuna watu wanataka kutumia hali ya sasa kujinufaisha,”alisema Lucas.

 

Kwa upande wake, mama lishe kwenye soko la Maili Moja, Aisha Juma alisema wanapata changamoto kutokana na bei hiyo, kwa kuwa wanauza chai kwa bei ndogo ya Sh 100 na maziwa kwa Sh 500 kwa kikombe.

 

Alisema kwa kuuza kwa bei hizo, hawapati faida, hivyo aliiomba serikali ishushe bei ya sukari ili iendane na hali halisi ya maisha, kwani wao wanawahudumia wananchi wa hali ya chini.

 

Muuzaji wa duka la bidhaa mbalimbali ikiwemo sukari, Kassimu Haji alisema sukari ilianza kupotea Februari, ambapo mfuko wa kilo 25 ulianza kupotea, ukabaki