News News

Back

VYAMA VYA USHIRIKA VYAHUDUMIA 229,000

06 May 2020
Nipashe
Image

JUMLA ya wateja 229,000 wamekuwa wakihudumiwa na vyama vya ushirika mkoani Mbeya kwa lengo la kujiongezea kipato kutokana na fursa mbalimbali ambazo wamekuwa wakipata zikiwamo za usimamizi bora wa soko la mazao yao.

 

Hayo yalielezwa jana na Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoani Mbeya, Angela Maganga,

wakati akizungumza gazeti hili kuhusiana na hali ya ustawi wa ushirika mkoani hapa kwa vyama

vya ushirika.

 

Alisema Vyama vya Msingi vya Kilimo na Masoko (AMCOS) ambavyo vimekuwa vikisimamia

mazao kama kakao, tumbaku na kahawa, vimekuwa na mchango mkubwa katika kusimamia

masoko ya uhakika ya wakulima katika soko, hivyo kuleta manufaa ya kiuchumi kwa wakulima

wanaouza mazao yao.

 

Akitolea mfano kwa zao la kokoa, Angela alisema bei ya zao hilo imepanda kutoka Sh. 1500 hadi

kufikia Sh. 5,000 hadi sasa kutokana na wakulima wengi kujenga utamaduni wa kuuza zao hilo

kwenye vyama vya ushirika.

 

“Hadi kufikia Desemba 2019 wakulima waliweza kuuza kakao kwenye vyama vyao vya ushirika

na kupata kiasi cha Sh. bilioni 59.8 na kuwa wengi wa madalali wameanza kuacha kazi hiyo ya udalali kutokana na kutokuwa na manufaa,” alisema Angela.

 

Alisema zao la tumbaku mpaka sasa kuna vyama 17 vya ushirika na kuwa kwa msimu wa

mwaka jana jumla ya kilo milioni 11 ziliuzwa kupitia vyama hivyo vya ushirika na kuwa kiasi cha

Sh. bilioni 40 zilipatikana na kugawiwa kwa wakulima hao.

 

Alisema uwapo wa vyama vya ushirika umekuwa ni mkombozi mkubwa kwa watu wengi hususan

wakulima kutokana na kuwapo kwa changamoto ya wakulima wengine kuuza mazao yao kwa

madalali ambao wamekuwa wakinunua mazao kwa bei ya dezo ambayo yamnufaishi mkulima.

 

Alisema mkoa wa Mbeya una jumla ya Saccos 212 ambazo zina hisa za Sh. bilioni 16, akiba kiasi

cha Sh. bilioni 19 na Amana kiasi cha Sh. bilioni tano.

 

Alisema mikopo iliyotolewa kwenye Saccos hizo ni kiasi cha Sh. bilioni 64 na kuwa kati ya

mikopo hiyo iliyotolewa kuna kiasi cha Sh. bilioni 40 ambazo zimerejeshwa mpaka sasa.