News News

Back

WAKULIMA KOROSHO WAJAZWA MABILIONI

16 Dec 2019
Habari Leo
Image

MKOA wa Pwani umewalipa wakulima wa zao la korosho Sh bilioni 60.6 kwa msimu wa mwaka 2018/19.

Pia korosho tani 46 za daraja la kwanza ziliuzwa kwa Sh 2571 na daraja la pili ziliuza tani 109 kwa Sh 2075 ambapo hadi Desemba jumla ya tani 765 zimeuzwa.

Akizungumza katika Kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC) kilichofanyika mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikilo alisema kwa wakulima ambao hawajalipwa serikali inaendelea na uhakiki ili kuwalipa walengwa.

“Korosho itakayolipwa ni ile itakayokuwa imepelekwa kwenye ghala kuu lakini zile zilizo kwenye vyama vya msingi vya ushirika watalipwa huko huko,” alisema Ndikilo.

Alisema hadi sasa kuna tani zaidi ya 6,000 ziko kwenye vyama vya ushirika vya msingi (Amcos) na korosho nyingine ziliharibika kutokana na  hali ya mvua na ukosefu wa magunia.

“Korosho nying ziko Amcos na hazina ubora unaotakiwa na iliamuliwa korosho zipimwe ubora kabla ya kupelekwa ghala".